Walidhani ni Al Shabab


Hofu yatanda chuo kikuu cha SAUT, Mwanza baada ya mwanafunzi mmoja mwenye asili ya kisomali kudhaniwa ni mfuasi wa al shabab. Tukio hili lilitokea Ijumaa ya tarehe 10 Aprili baada ya taarifa kutanda mitandao ya kijamii hasa whatsapp kuwa magaidi wa al shabab, ambao asili yao ni somalia, walikuwa na mpango wakufanya ugaidi Mwanza siku hiyo.

Inasemekana mwanafunzi huyo mwenye asili ya kisomali aliingia darasa moja la BBA (Bachelor of Business Administration) ambamo walikuwa wakifanya mtihani wanafunzi. Baada ya kuingia darasani mwalimu alijaribu kumuuliza maswali lakini hakujibu swali hata moja. Inasemekana mwalimu huyo ilibidi aulize darasa kama wanamfahamu na darasa walijibu hawamjui na wala hawajawahi kumwona.
Ndipo mwalimu uzalendo ukamshinda na kutimua mbio huku wanafunzi nao wakitimua mbio na baadhi yao kuumizana.

Walinzi walifika na kumtia nguvuni mwanafunzi huyo. Ila habari za kuaminika zinasema kwamba huenda mwanafunzi huyo alikuwa ana “carry” au alipotea darasa hali iliyopelekea hata wanafunzi wenzake kushindwa kumtambua na kuzua hali ya taharuki.


Walinzi wakimuhoji kijana huyu

Kijana akisindikizwa kutoka darasani

1 comment:

  1. Casinos Near DC - DrMCD
    Casinos near DC. Find out more about the city, 광주 출장마사지 casinos, 부천 출장샵 restaurants, nightlife, dining 계룡 출장마사지 options, and nearby 사설 토토 사이트 attractions in the area. 밀양 출장샵 More about the city.

    ReplyDelete